Majeshi ya Afghanistan yamefanikiwa kuutwaa tena mji wa Kunduz kaskazini mwa nchi hiyo uliokuwa umetekwa na wapiganaji wa kikundi cha Taliban.
Maafisa wanasema oparesheni iliyofanywa wakati wa usiku ilishuhudia majeshi ya yakiteka tena maeneo ya serikali katika mji huo na kusababisha maafa makubwa kwa wapiganaji hao.
Hata hivyo hakujawa na taarifa yoyote kutoka kwa kikundi cha Taliban lakini mapigano inaseekana yanaendelea na kutekwa kwa mji huo lilikuwa pigo kubwa kwa Rais ASHRAF GHANI.
Kumekuwa na shinikizo kwa Bwana GHANI ambaye ameadhimisha mwaka mmoja tangu ashike madaraka kujiuzulu kwa kushindwa kutimiza majukumu yake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment