Image
Image

CCM yakiri kupoteza majimbo manne ya uchaguzi na halmashauri.

Chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya kimekiri na kukubali kupoteza majimbo manne ya uchaguzi na halmashauri mbili ambazo zimenyakuliwa na vyama vya upinzani kwenye uchaguzi mkuu uliofanyikatarehe  25, mwezi uliopita.
Aidha chama hicho Mkoani Mbeya kimempongeza Rais Mteule wa awamu ya tano,  Dakta  JOHN POMBE MAGUFULI kwa kutangazwa mshindi wa ngazi ya urais kwenye uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya, GODFREY  ZAMBI ametoa tamko hilo kwa niaba ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya makada  wa CCM wamesema kuwa ushindi wa  Dakta  MAGUFULI ni ushindi wa Watanzania wote kwa kuwa ni mtu mwadilifu na mwenye uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na tabia yake ya kupenda kuchapa kazi.
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa wanamtarajia Rais MAGUFULI kuteua wasaidizi wake walio makini ili akidhi  matarajio ya wanananchi wametoa hadhari kwa viongozi wazembe serikalini kuwa wajiandae kwa mabadiliko na kuanza kujituma kufanya kazi baada ya kuapishwa kwa Dakta  MAGUFULI  Alhamisi ijayo kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment