Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Balozi KHAMIS KAGASHEKI ametoa hadhari kwa baadhi ya watu wanotumia mitandao ya kijamii na kumtuhumu kuwa baada ya kushindwa kupata nafasi ya ubunge ameondoa baadhi ya vitu alivyovitekeleza akiwa mbunge wa jimbo hilo.
Vitu anavyodaiwa kuviondoa ni pamoja na kuondoa mtengo wa radi katika Shule ya Msingi Kibeta , Televisheni ya wanchi ya Uhru Platfom, gari la kubebea wagonjwa na kuzima umeme katika Soko Kuu la Kashai Mjini Bukoba.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Bukoba, Balozi KAGASHEKI amesema hajaondoa kitu chochote alichokitekeleza katiika jimbo hilo bali hayo nimaneno yanay enezwa na baadhi ya watu waliopanga kumchafua na kueneza chuku dhidi yake.
Amewataka watu wanaotumia mitandao kumchafua katika mitandao ya jamii kuacha mara moja kwani hatosita kuwachukulia sheria wale wote wanaomchafua bila sababu yoyote.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment