Twiga Stars iliingia kambini Oktoba 29, katika hosteli za Shirikisho
zilizopo Karume, ina kikosi cha wachezaji 22 wanaofanya mazoezi asubuhi na
jioni katika uwanja wa Karume.
Mchezo dhidi ya Malawi ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa, ambao kocha
Kaijage atautumia kuangalia maendeleo ya wachezaji wake kwa ajili ya maandalizi
ya micheo ya kimataifa.
Wachezaji waliopo kambini ni Asha Rashid, Estha Chaburuma, Fatuma
Bushiri, Fatuma Omari, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Amina
Ally, Fatuma Issa, Belina Julius, Happines Hezron na Donizia Daniel.
Wengine ni Maimuma Hamisi, Stumai Abdallah, Anna Hebron, Anastazia
Anthony, Shelder Boniface, Wema Richard, Tumaini Michael, Jane Cloudy, Saada
Ramadhani na Sofia Mwasikili.
0 comments:
Post a Comment