Mawaziri wa Mambo ya Ndani na wale wa sheria wa Umoja wa Ulaya leo hii
wanafanya mkutano wa dharura wenye lengo la kuzidisha ulinzi katika
maeneo ya mipaka yake baada ya kuuwawa kwa kiongozi wa mashambulizi ya
Paris.
Abdelhamid Abaaoud, raia wa Ubeligiji mwinye asili ya Morocco,
anatuhumiwa kuwa muhusika aliyepanga mashambilizi ambayo yalisababisha
watu 129 wapoteze maisha, kwa niaba ya kundi la Dola la Kiislamu,
aliuwawa jana kutokana na shambulio la polisi katika jengo moja huko
kaskazini mwa jiji la Paris.
Kuna fikra kwamba kijana huyo wa umri wa miaka 28 alikuwa nchini Syria,
ambako alipata uwezo wa kupanga mashambulizi dhidi ya mataifa ya
Magharibi. Kwa hivyo uwepo wake nchini Ufaransa unaongeza unazusha
maswali kuhusu namna Ulaya inavyoshughulikia mgogoro mkubwa kabisa wa
kikanda wa wimbi la wahamiaji tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya
Dunia.
Kauli ya mawaziri wa mambo ya mambo ya ndani.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema taifa
lake halijapata taarifa yoyote ya onyo kutoka mataifa wanachama kwamba
Abaaoud yupo katika maeneo ya kanda hiyo, na kupasawa kanda hiyo kuwa
macho mara moja, kujipanga na kujilinda dhidi ya kitisho cha ugaidi.
Akiwasikili katika eneo la mkutano, nae wa Mambo ya Ndani wa Uingereza
Theresa May alinikuliwa akisema "Ningalipenda kuona mataifa yote
wanachama, wanajikita katika kuboresha hatua na adhabu kwa wote wenye
kuhusika na usafirishaji haramu wa binaadamu na silaha, na majina ya
abiria yahifadhiwe katika kumbukumbu. Tunahitaji maendeleo ya hatua hiyo
haraka, mazungumzo yamechukua muda mrefu, yanapaswa kufikiwa
hitimisho".
Mawaziri wa mambo ya ndani na wa sheria watajadili namna ya kuhimarisha
ukaguzi katika maeneo ya mipaka kwa wasafiri wote katika mataifa 26
yaliyo katika umoja wa Schengen kama hatua za dharura.
Kitisho cha wakimbizi
Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Vals alisema baadhi ya wauwaji wa mkasa
wa Paris walichukulia kigezo cha mgogoro wa uhamiaji barani Ulaya
kuingia katika eneo hilo pasipo kubainika na kuonya mataifa yaliyo
ukanda wa Schengen, kwamba yanaweza kuwa katika hatari endapo
hayatodhibiti ulinzi katika mipaka yake.
Abaaoud inamuungano na Syria na kandoni mwa mwili wake kulikutwa
pasiposi ya Syria ya mshambuliaji mmoja ambae jambo lilizusha wasiwasi
kwamba mipiganiaji huyo wa vita vya jihadi aliingia Ulaya kwa kigezo cha
ukimbizi katika taifa hilo lililigubikwa na vita, kwa lengo la kupanga
njama za kufanya mashambulizi.
Nchini Marekani, Bunge lililogubikwa na chama cha Republican, walipiga
kura ya kupiga marufuku wakimbizi wa Syria na Iraq kuingia Marekani
mpaka hatua madhubuti za ukaguzi zitakapoimarishwa. Na Urusi yenyewe
bado ipo katika tafakari baada ya mkasa wa ndege yake ya abiria
kudunguliwa nchini Misri na kusababisha vifo vya watu wote 224
walikuwemo katika ndege hiyo, katika shambulizi lingine linalodaiwa
kufanywa na kundi la Dola la Kiislamu. Mabaraza yote mawili ya bunge la
taifa hilo yatafanya mikutano mkubwa leo hii ya kujadili namna ya
kukabiliana na ugaidi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment