Rais Dakta JOHN MAGUFULI leo amemwapisha Mbunge wa Ruangwa, MAJALIWA KASIM MAJALIWA kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hafla hiyo fupi imefanyika kwenye viwanja vya Ikulu ndogo Chamwino Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Viongozi wengine ni pamoja na Makamu wa Rais, SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dakta ALI MOHAMMED SHEIN, Jaji Mkuu, Mheshimiwa MOHAMMED CHANDE OTHMAN, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JOB NDUGAI na Spika wa Baraza la Wawakilishi, PANDU AMEIR KIFICHO.
Leo alasiri Rais MAGUFULI anatarajiwa kulizindua rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baada ya uzinduzi huo inatarajiwa kuwa Bunge litaahirishwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment