Image
Image

Watu wenye silaha washambulia hoteli Mali.

Watu wenye silaha wameshambulia hoteli ya Radisson Blu katika mji mkuu wa Mali, Bamako, ripoti zinasema.
"Kuna dalili kwamba hili ni jaribio la kuwachukua watu mateka. Polisi wako hapo na wamezingira eneo hilo," duru za kiusalama zimeeleza shirika la habari la Reuters.
Milio ya risasi inasikika kutoka nje ya hoteli hiyo yenye vyumba 190, shirika la habari la AFP linasema.
Mwandishi wa BBC Afrique Abdourahmane Dia anasema hoteli hiyo, inayomilikiwa na Wamarekani, hutumiwa sana na raia wa kigeni wanaofanya kazi nchini Mali.
Kampuni inayomiliki hoteli hiyo imesema juhudi zinafanywa kudhibiti hali.
"Maafisa wetu wanawasiliana na maafisa wa serikali kupata usaidizi kurejesha usalama na hali ya kawaida hotelini," kampuni hiyo ya Rezidor Hotel Group imesema, na kuongeza kwamba kulikuwa na wageni 140 hotelini ambao wamezuiliwa na "watu wawili".
Agosti, wapiganaji wa Kiislamu waliua watu 13, wakiwemo wafanyakazi watano wa UN, baada ya kushikilia mateka watu katika mji wa Sevare, katikati mwa Mali.
Ubalozi wa Marekani mjini Bamako umeandika kwenye Twitter kwamba unafahamu kuhusu shambulio hilo na kuwashauri wafanyakazi wake pahala salama nao raia wawasiliane na familia.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment