WAZIRI Mkuu mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, ambaye ameapishwa na Rais wa Tanzania na kuwa waziri kamili Mh.Kassim Majaliwa,amewaahidi makubwa wanamichezo, akisema ni eneo analolifahamu vyema na
wasihofu katika hilo. Kutokana na hali hiyo amesema atamshauri Rais John
Magufuli kumteua Waziri atakayeshughulikia michezo yule ambaye ana
uelewa mpana zaidi wa mambo ya michezo.
“Mimi ni kocha mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ni
mkufunzi wa TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), ni kocha niliyesomea hasa
na pia kuifanya hiyo kazi. “Najua wanamichezo wanahitaji mambo gani,
naelewa sasa michezo ni ajira pia ni afya, hilo ni eneo langu.
“Nataka kupitia michezo tujitangaze, wanamichezo wawe mabalozi wetu
wazuri, wasihofu mwanamichezo mwenzao nipo".
Licha ya kuwa Kocha Mkuu wa Bunge SC, Majaliwa amepata kuwa kocha wa
timu mbalimbali mkoani Mtwara, pia amekuwa mkufunzi wa michezo na
alikuwa kocha wa timu mbalimbali katika mashindano ya shule za msingi
(Umitashumta) na sekondari (Umisseta) miaka ya nyuma.
Majaliwa anakuwa Waziri Mkuu wa 11,waliomtangulia wakiwa Mwalimu
Julius Nyerere, Rashidi Kawawa, Edward Sokoine (wote marehemu), Cleopa
Msuya, Dk Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba, Dk John Malecela, Frederick
Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda.
Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk Hamisi Kigwangwala alisifu uteuzi huo na
kwamba ni furaha kubwa kwa wanamichezo kwani Majaliwa ni mwanamichezo
hasa na anayeijua vyema michezo. Hata hivyo, Kigwangwala alieleza hofu
yake kama ataendelea kupata fursa ya kufanya mazoezi na wabunge na pia
ataendelea kuwa kocha wa timu ya Bunge SC.
Mbunge wa Kilolo, ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu
katika timu mbalimbali na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Venance Mwamoto,
alisifu uteuzi wa Waziri Mkuu mwanamichezo.
“Huyu ni mwanamichezo halisi, sio tu kuipenda bali pia kucheza,
tunamuahidi ushirikiano mkubwa sisi wanamichezo,” alisema Mwamoto na
kumpongeza Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa uteuzi huo. Majaliwa
aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa akishughulikia elimu katika Serikali ya Awamu ya Nne,
alithibi-
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment