SHIRIKA la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika (WiLDAF)
na wadau mbalimbali wanaopinga ukatili wa kijinsia wameiomba serikali
kuboresha miundombinu kwa watoto wa shule iwe rafiki ili kupunguza
vitendo vya ukatili.
Miundombinu hiyo ni kuwepo kwa vyoo bora, mabweni ya wanafunzi,
madawati, usafiri, uzio wa kuzunguka shule kwa ajili ya ustawi wa
wanafunzi wa shule. Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi wa WiLDAF, Judith Odinga alisema kutokuwepo kwa
miundombinu bora kunachangia ongezeko la ukatili wa jinsia.
Odunga alisema mazingira yasiyo salama kwa watoto shuleni, yana
madhara makubwa na kwamba wanaamini kuondolewa kwa vikwazo, hivyo
kutapunguza ukatili wa kijinsia kwa watoto na kuleta usawa wa kijinsi
kwa watoto wa kike na wa kiume.
Alisema katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kaulimbiu yao
ni ‘Funguka, Chukua hatua mlinde mtoto apate elimu’. Maadhimisho hayo
yatafanyika kesho hadi Desemba 10 na yatazinduliwa kwa maandamano
kuanzia Sinza darajani hadi Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na Chuo cha Tiba Muhimbili (MUHAS)
kwa kushirikiana na WiLDAF, alisema umetambua athari zinazochangia
ukatili wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na wazazi kutowajali watoto na
adhabu kali.
Aidha, adhabu ya viboko inahusishwa kama moja ya aina za ukatili
dhidi ya watoto na kwamba inaathiri maendeleo ya elimu ya watoto katika
Taifa. Kutokana na hali hiyo, shirika hilo limeiomba serikali kufuta
adhabu ya viboko mashuleni na kuomba walimu watumie njia mbadala ya
kuwaadhibu wanafunzi.
Alisema ni lazima kutengeneza muongozo wa utekelezaji wa sera ya
elimu ya mwaka 2014, utakaoelekeza upatikanaji wa elimu ya msingi iliyo
bora na salama na kuunda mabaraza yatakayosimamia malalamiko ya
wanafunzi mashuleni.
“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Katiba na Sheria
zitunge sheria kuthibiti ukatili majumbani na kubadilisha Sheria ya Ndoa
ya mwaka 1971, inayoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kuolewa,”
alifafanua Odunga.
Home
News
WiLDAF yaiomba serikali kuboresha miundombinu kwa watoto wa shule ili kupunguza ukatili wa kijinsia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment