Image
Image

Agizo la Rais Magufuli kudhibiti wizi wa dawa hospitali limeanza kutekelezwa

Utekelezaji wa agizo  la Rais, Dakta  JOHN POMBE MAGUFULI  la  kuhakikisha  hospitali  zote za  rufaa zinakuwa na maduka  ya dawa yanayosimamiwa na Bohari  Kuu ya Dawa limeanza  kutekelezwa  katika  Hosipitali  ya Mkoa  wa  Arusha - Mount  Meru  na  tatizo  la  ukosefu wa dawa katika hosipitali  hiyo linatarajiwa kuisha baada  ya  wiki  tatu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari  Kuu ya Dawa  nchini, LAUREAN RUGAMBWA amesema baada ya  kukamilisha  zoezi hilo  katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili  sasa utekelezaji  unahamia  mikoani  wakianzia  na  Mkoa wa Arusha.
Katibu Tawala  wa Mkoa  wa Arusha, ADO  MAPUNDA  amesema  utekelezaji  wa maelekezo  hayo  unakwenda  pamoja na kuendelea  kuboresha  huduma nyingine  ikiwemo miundombinu ya utoaji wa  huduma  katika  hospitali   hiyo  ya mkoa  na pia za wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,FELEXS  NTEBENDA  KIJIKO amesema  hatua  hiyo ni mwanzo wa  kazi kubwa  inayowakabili   watendaji   wa  ngazi  zote  ya kukomesha uzembe,wizi  wa dawa   na   matatizo  mengine   yanayochangiwa  na  kukosekana  kwa  uwajibikaji.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment