Mtuhumiwa mkuu katika kesi ya mauwaji yaliyofanywa na wafuasi wa chama
cha NSU,Beate Zschäpe ameamua hatimae kufumbua mdomo mahakamani.Anadai
"hana alichokiona wala kukisikia".Familia za wahanga hawajaridhika.
Taarifa kwamba Beate Zschäpe ameamua hatimae kuzungumza zilienea kufumba
na kufumbua.Umati wa watu walijazana katika uwanja wa Stigmeier mjini
Munich tangu jana usiku.Ndani ya ukumbi wa mahakama,viti vyote 100
vilijaa tangu waandishi habari mpaka watu wa kawaida .Familia za wahanga
pia walihudhuria wakijiwekea matumaini pengine Beate Zschäpe angefichua
ukweli na pengine kuomba radhi kwa yaliyotokea.
Hakuna kilichotokea.Sio yeye aliyezungumza,bali wakili Mathias
Grasel-mmojawapo wa mawakili wawili wepya aliopewa na serikali -huyo
ndie aliyesimama kusoma kile alichotaka kukisema Beate Zschäpe
mahakamani."Sijahusishwa si katika maandalizi na wala si katika
kuyatekeleza mauwaji hayo yaliyofanyika kati ya mwaka 2000 na
2007-amesema Beate Zschäpe katika taarifa hiyo.Hata hivyo anasema
anajibebesha jukumu la kiroho kwa kushindwa kuwashawishi washiriki
wawili wakati ule ,Uwe Böhnhard na Uwe Mundlos wazuwie mauwaji hayo na
ndio maana anasema "anawaomba radhi kwa dhati wahanga wote."
Familia za wahanga hawajaridhika na samaha ya Zschäpe.
Binti ya mhanga mmojawapo wa mauwaji hayo amekataa samahani za Beate
Zschäpe."Alichokisema Zschäpe hakina maana yoyote" amesema Gamze
Kubasikm,binti ya mwenyeduka mmoja aliyeuliwa Dortmund mwaka 2006-Mehmet
Kubasik.
Mwanaharakati huyo wa zamani wa siasa kali za mrengo wa kulia
alijitenganisha na mawakili wake wa awali waliokuwa wakimshauri asiseme
kitu mahakamani ili kuepusha asijite matatani.
Beate Zschäpe anafikishwa mahakamani tangu May mwaka 2013 kwa makosa ya
kushiriki katika mauwaji ya watu 10,kufanya mashambulio mawili ya mabomu
dhidi ya wageni na kuvunja benki mara kumi.
Washiriki wake wawili wakubwa wamefariki dunia.
Beate Zschäpe ndie pekee aliyesalimika kati ya kundi la watu
watatu,wenzake wawili,Uwe Böhnhardt na Uwe Mundlos walipatikana
wameuliwa kwa kupigwa risasi,polisi ilipotaka kwenda kuwakamata mwishoni
mwa mwaka 2011 baada ya kuvunja benki moja mashariki ya Ujerumani.
Wahanga wanane waliouliwa na kundi hilo walikuwa na asili ya kituruki.
Kisa hicho kiliitikisa Ujerumani kwasababu kundi hilo lilikuwa likifanya
vituko vyake kwa miaka kadhaa bila ya hofu-hali iliyozusha suala la
uzembe katika idara ya upelelezi wa ndani.Mbali na Beate Zschäpe,wafuasi
wanne wengine wa wananzi mambo leo wanashitakiwa kwa dhana za
kuwasaidia kundi hilo la watu watatu walioishi mafichoni kwa muda wa
miaka 13.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment