Image
Image

Chagonja atupwa zimamoto na kuwa kamishna mpya wa jeshi hilo la zimamoto na uokoaji.


Rais Dk. John Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya utendaji ndani ya Jeshi la Polisi kwa kumhamisha Kamishina wa Operesheni na Mafunzo,CP Paul Chagonja na kuwa Kamishina mpya wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Rais Magufuli amesemakuwa amefanya mavbadiliko madogo ndani ya Jeshi la polisi kwani ni mabadiliko ya kawaida tu.
“Kama unavyojua Rais Magufuli anakwenda na falsafa yake ya ‘Hapa Kazi Tu’ inaonekana amedhamiria kuboresha maeneo yote…huwezi kujua leo wizara hii kesho wizara nyingine, tunapaswa kujiandaa kila kukicha ndugu yangu,”kilisema chanzo chetu cha habari.
Kamishina Chagonja, amekuwa katika nafasi hiyo kwa muda mrefu tangu utawala wa aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu Said Mwema.
“Chagonja ametumikia nafasi hii muda mrefu kidogo kuanzia wakati ule wa IGP Mwema mpaka sasa IGP Mangu (Ernest), naamini kutokana na uzoefu wake imeonekana anafaa kwenda huko,”kilisema chanzo hicho.
Kamishina Chagonja katika utumishi wake, amewahi kuwa Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi na baadae Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es Salaam.
Januari 22, 2013, Rais mstaafu Jakaya Kikwete alimteua Pius Makuru Nyambacha kuwa Kamishina Jenerali wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.
Hivi sasa nafasi hiyo inakaimiwa na Kamishina Jenerali Rogatius Kipali.
Alipotafutwa msemaji wa kikosi hicho, Puyo Nzalayaimisi simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Hata hivyo Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alipotafutwa kuzungumzia mabadiliko hakuweza kupatikana kutokana na simu yake kuita bila bila kupokewa.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment