Mahakama ya Juu nchini Afrika Kusini imempata
mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius na hatia ya mauaji.
Mahakama hiyo imekubali rufaa iliwasilishwa na
upande wa mashtaka ikitaka Pistorius apatikane na hatia ya mauaji, ambayo
adhabu yake ni kali zaidi kuliko ya kuua bila kukusudia.
Jaji Lorimer Leach amesema mwanariadha huyo anafaa
kurejeshwa kwa jaji aliyemhukumu ili apokee adhabu ya kosa la mauaji.
Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp
Februari 2013 baada ya kufyatua risasi kupitia mlango
Amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani baada ya
kukaa mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Awali, ilikuwa imeripotiwa kimakosa kwamba rufaa
hiyo ilikuwa imetupwa na angeendelea kutumia kifungo cha kuua bila kukusudia.
Pistorius alifungwa jela miaka mitano mwaka 2014
baada ya kupatikana na kosa hilo la kuua bila kukusudia.
wa choo.
0 comments:
Post a Comment