Mkuu wa Mkoa wa Kagera,JOHN MO NGELLA amewataka watumishi wote manispaa hiyo kufunga ofisi na kuingia mtaani kufanya usafi wa mazingira kutokana uzembe uliofanywa na Maofisa Afya wa manispaa hiyo kwa kushindwa kusimamia kwa ukamilifu suala usafia wa mazingira.
Ametoa agizo hilo baada ya kupokea vifaa vya usafi vilivyotolewa na Shirika la Hisani la World Vision kwa lengo la kukabilana na uogonjwa wa Kipindupindu ambao umekuwa tishio kwa wananchi .
Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera ameamuru watumishi wote wa Manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na wananchi kuwajibika kufanya usafi wa mazingira katika Mtaa wa Bunena,Kashabo na Buyekela,mitaa ambayo imetajwa kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa Kipindupindu kutoka na na ongezeko la uchafu katika maeneo hayo .
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya,Dakta HAMZA MUGULA amesema jitihada za kupambana na ugnjwa huo zinaendelea kwa kasi kubwa na kuongeza kuwa taangu tarehe 13 Oktoba mwaka huu hadi sasa wamepokea wangonjwa wa Kipindupindu zaidi ya miamoja na kati hao wawili walipoteza maisha.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment