Mali imewekwa rasmi tangu Jumanne hii katika hali ya
tahadhari hadi mwanzoni mwa mwezi Januari mwakani, ikiwa ni kwa mara ya pili
tangu shambulio dhidi ya hoteli moja ya kifahari mjini Bamako mwezi Novemba,
wakati ambapo wanajihadi kadhaa "wameangamizwa" na jeshi la Ufaransa.
Aidha, katika ripoti, kitengo cha Haki za Binadamu cha
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa UN nchini Mali (Minusma) kimelaani "ukiukwaji
mkubwa wa sheria za kimataifa" katika mashambulizi ya kijiji kimoja,
kaskazini mwa nchi. Mashambulizi ambayo yanadaiwa kutekelezwa na makundi ya Azawad
(CMA, kundi la waasi lenye watu wengi kutoka jamii ya Watuareg), na wakati
kijiji hicho kilipowekwa chini ya himaya ya vikosi vya serikali.
Raia wawili waliuawa wakati wa shambulio lililoendeshwa na
waasi wa CMA katika kijiji cha Tin Hama, na siku iliyofuata, raia wengine sita
waliuawa, na jamii, ambayo inatuhumiwa kuunga mkono waasi, ilifukuzwa kwa
vitisho. Karibu watu 230, kulingana na ripoti hiyo, ilithibitisha taarifa
zilizokusanywa wakati huo baina ya wahusika wakuu.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) unalaani
ukiukaji wa sheria za kimataifa na makundi ya waasi na kusikitishwa hasa kuona
hakuna uchunguzi wa mahakama ulioanzishwa, na vile vile upande wa vikosi vya
kijeshi, na kudai uchunguzi wa serikali "kuhusu tabia ya askari walio kuwepo
katika kijiji cha Tin Hama tarehe 20 na 21 Mei, na ushiriki wao, kwa njia moja
au nyingne "katika mauaji hayo
Mapigano kati ya kundi la waasi la CMA na makundi yanaounga
mkono serikali ya Bamako yameendelea licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani
mwezi Mei hadi Juni, lakini walisitisha tangu wakati huo hitimisho la
"mkataba wa heshima" kati ya wadau wote katika mchakato huo Oktoba
16, baada ya wiki tatu ya mikutano katika mji wa Anefis, kaskazini-mashariki
mwa Mali.
0 comments:
Post a Comment