Mserbia alisema jana kuwa kikosi cha Stars amekishuhudia kwenye
michuano hiyo kikiwa na ubora kwenye kila idara na anakipa nafasi kubwa
ya kutinga fainali.
“Katika hatua ya robo-fainali niliomba Mungu tusikutane na
Kilimanjaro Stars, ndiyo timu ngumu ninayoiona mpaka sasa. Ina mabeki
makini, viungo wabunifu na washambuliaji wenye kasi na uwezo mzuri wa
kushambulia,” alisema Micho.
Kocha huyo wa zamani wa Yanga, alisema kuwa safu ya kiungo ya Stars
ndiyo inayofanya kazi kubwa zaidi kiasi cha kuifanya timu hiyo
kukusanya pointi saba katika mechi tatu za hatua ya makundi.
Uganda itacheza mechi yake ya robo-fainali ya michuano hiyo dhidi
ya timu mwalikwa, Malawi kwenye Uwanja wa Addis Ababa kabla ya Stars
kuwakabili wenyeji, timu ya taifa ya Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment