WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip
Mpango amesema kamwe hatapenda kuwa waziri ombaomba wa fedha, bali atahakikisha
anaelekeza nguvu katika kukusanya kodi ili nchi iweze kujitosheleza kwa mapato
ya ndani.
Aidha, amesema atahakikisha mifumo ya
kodi inakuwa rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili wasikimbie kulipa
kodi, huku akiahidi kuangalia jinsi ya kuachana na kodi zenye kero kwa
Watanzania.
Aliyasema hayo jana jijini Dar es
Salaam wakati alikabidhi ofisi kwa Kaimu Kamishna Mkuu mpya wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata. Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha
wiki iliyopita, Dk Mpango alikuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, wakati Kidata
alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
“Sipendi kuwa waziri wa kuombaomba
hivyo nitaelekeza nguvu zangu katika ukusanyaji kodi na kuona nchi yetu
inajitegemea kwa mapato ya ndani kwa kiasi kikubwa, lakini ili kufanya hivyo ni
lazima kuziba mianya ya mapato…” alisema Dk Mpango.
0 comments:
Post a Comment