“Watendaji
ni kiungo muhimu kwa waziri kutekeleza majukumu yake, ni matumaini yangu mtampa
ushirikiano katika hili,” alisema.
Nyalandu
alisema ushirikiano huo utawezesha rasilimali za nchi kama misitu na wanyama
kuendelea kuwapo na kutumika kwa njia endelevu.
Alisema
umuhimu wa wizara kuendelea kutangaza vivutio vya utalii ili kuhakikisha
malengo katika sekta hiyo unazidi kufikiwa.
“Wizara
hii ina watendaji wema na wanaojitolea kutimiza majukumu yao, kuna askari wa
wanyamapori na misitu wanaofanya kazi kwa weledi,” alisema Nyalandu.
Kwa
upande wake, Waziri Maghembe alisema wizara yake imejipanga kufanya kazi kwa
kasi zaidi na kuendeleza yale ambayo yalifanywa na mtangulizi wake.
“Ninatambua
mwenzangu alifanya kazi kubwa ya kuendeleza na kusimamia wizara… na mimi
kwa kushirikiana na watendaji tutafanya kazi na kuzidi kuleta mafanikio,”
alisema Profesa Maghembe.
Alitaja
baadhi ya maeneo yatakayopewa kipaumbele ni kukomesha wizi wa magogo na vita
dhidi ya ujangili wa wanyama pori.
“Watu
walikuwa wanavuna magogo na kujifanya kama yanatoka nchi jirani ya Zambia,
ulipambana na kutengeneza ushirikiano na nchi hizo…tutaiga mfano wako,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment