MAKAMU wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan amezitaka taasisi mbalimbali za umma na za kiraia kuanzisha
kampeni maalum ya kukuza maadili nchini.
Amesema hayo kwenye maadhumisho ya nane ya kitaifa
ya Haki za Binaadamu yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kuongeza
kuwa maadili ni chanzo cha huchochea utu na haki za binaadamu.
Amesema kuwa, kulinda na kuheshimu haki za binaadamu
ni wajibu wa kila mtu katika jamii ambapo serikali, familia au kaya na mtu
mmoja mmoja kuhusika kuzilinda.
Amesema Serikali ya Awamu ya Nne imepokea kiporo cha
Katiba na kwamba serikali yake itaheshimu maoni ya wananchi yaliyokusanywa na
kuhakisha kuwa, yanazingatua haki za binaadamu.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala
Bora, Bahame Nyanduga amesema kuwa haki za binaadamu zimeimarika nchini licha
ya changamoto za mauaji yanayotokana na imani za kishirikina pamoja na mauaji
ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), wazee, ukatili dhidi ya watoto na
jinsia, mauaji ya kujichukulia sheria mkononi na uwelewa mdogo wa haki za
binaadamu.
Maadhimisho ya mwaka huu ni ya nane tangu
yalipopitishwa na kuadhimishwa mwaka 2008 ambapo Tanzania inaungana na mataifa
mengine katika kuadhimisha siku hiyo na kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ‘Haki
zetu, Uhuru wetu Daima’
0 comments:
Post a Comment