Bunge la Uingereza hii leo linatarajia kupiga kura kuiruhusu nchi yao
kujiunga na mapambano dhidi ya kundi la dola la kiisilamu la IS nchini
Syria.
Waziri mkuu wa Uingereza , David Cameron ambaye ari yake ya kuliangamiza
kundi hilo la dola la kiisilamu imeongezeka zaidi hasa baada ya
mashambulizi ya mjini Paris anatarajiwa kuongoza mjadala bungeni
unaotarajiwa kuchukua zaidi ya saa kumi katika kuelekea upigaji kura
huo.
Mawaziri nchi humo wanaimani kwamba wabunge watapiga kura ya ndiyo
kuunga mkono hatua hiyo hali ambayo inaashiria kuwa ndege za kijeshi za
Uingereza zitaanza mashambulizi kulilenga kundi hilo la dola la
kiisilamu huko nchini Syria kabla ya kufikia mwisho wa juma hili.
Cameron amesisitiza ya kuwa hatua za kijeshi zinahitajika sasa ili
kuzuia mashambulizi kama yale ya yaliyoua watu 130 mjini Paris mwezi
uliopita, lakini pia akiongeza kuwa hatua hiyo itaenda sambamba na
juhudi za kidiplomasia zinazoendelea sasa katika kushughulkikia mgogoro
wa Syria.
" Nitajitahidi kujenga hoja na nina imani kuwa wabunge wengi kutoka
katika vyama vyote wataniunga mkono "alisema waziri mkuu Cameron katika
kuelekea kura hiyo:
Hata hivyo baadhi ya wataalamu wa masuala ya kisiasa na ya kivita,
wanasema wabunge kadhaa na raia wa kawaida wanaonekana kuwa na mashaka.
Makundi ya watu wanaopinga mambo yanayohusiana vita tayari wameandamana
kuonyesha kutounga mkono hatua hiyo.
Baadhi ya wachambuzi wanauona hatua hii ya uingereza kutaka kushirika
katika kampeni dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu kama hatua moja
wapo ya kuwaunga mkono bega kwa bega washirika wake ambao ni mataifa ya
Marekani na Ufaransa.
" Cameron kwa sasa anaona ni lazima aiunge mkono Ufaransa katika kipindi
hiki inachokabiliana na tatazo la ugaidi " alisema Ben Berry ambaye ni
mmoja wa washauri katika siasa za kimataifa.
Tayari Uingereza imekuwa ikishiriki katika mashambulizi ya anga dhidi ya
kundi la dola la kiisilamu nchini Iraq kampeni ambayo ilianza tangu
mwaka jana.
Aidha inaarifiwa pia kuwa Uingereza imeombwa nawashirika wake yakiwemo
mataifa ya Ufaransa na Marekani kujiunga kikamlifu katika kampeni hiyo
ya mashambulizi dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu.
Tayari kumekuwepo na maandamanao nchini humo kupinga hatua ya kivita
dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu kama anavyosema mmmoja wa watu
walioshiriki katika maandamano hayo
Chama cha Labour chagawanyika kuhusiana na hatua
Hatua hii ya Cameron inakuja mnamo wakati chama kikuu cha upinzani cha
Labour nchini humo kikiwapa uhuru wa kuamua wabunge wa chama hicho
katika kuunga mkono au kutounga mkono uamuzi huo pasipo shinikizo lolote
kutokana na msimamo wa kiongozi mkuu wa chama cha Labor Jeremy Corbyn
anayeonekana kupinga hatua hiyo .
" Tunataka kuwaua watu nchini mwao kwa kutumia mabomu yetu , tafadhali
pigeni kura ya kutounga mkono hatua hii ya serikali dhidi ya
mashambulizi ya nchini Syria" alisema kiongozi huyo wa chama cha Labor
Hata hivyo hatua hii ya kutopata shinikizo kutoka katika chama chao
inaonyesha kuwa wabunge wa chama cha Labour ambao wanataka hatua za
kijeshi zichukuliwe dhidi ya kundi hilo la dola la kiisilamu watapiga
kura ya ndiyo hali ambayo inaonesha kuwa waziri mkuu Cameron atapata
ushindi mkubwa katika azima yake hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment