Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kahama
mjini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha
Demokrasia na maendeleo Bw.James Lembeli dhidi ya mgombea ubunge kwa tiketi ya
chama cha mapinduzi Jumanne Kishimba imeanza kusikilizwa katika mahakama kuu
kanda ya Shinyanga.
Kesi hiyo namba moja ya uchaguzi 2015 iliyoanza
kuunguruma katika Mahakama kuu kanda ya Shinyanga imeshindwa kuendelea baada ya
wakili wa upande wa mlalamikiwa Bw.Konstantini Mutalemwa akisaidiwa na pendo
makondo wakili mfawidhi mkuu wa serikali Shinyanga na Solomoni Rwenge wakili wa
serikali mwandamizi Shinyanga kuwasilisha pingamizi kuwa kifungu cha nane
katika hati ya mlalamikaji chenye vipengele A,B,C na D kinacholalamikia
matumizi ya rushwa katika zoezi la uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Kahama
mjini kiondolewe kwakuwa hakiko sawasawa kisheria.
Kwa upande wake wakili wa mlalamikaji Bw.Mpale Mpoki
amesema kulingana na sheria ya uchaguzi Tanzania haoni sababu ya kuletwa
pingamizi la kuondolewa kifungu hicho ambacho katika maudhui yake yamebeba sababu
za msingi zinazohusiana na rushwa iliyokuwa ikitumika wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita huku
mlalamikaji Bw.James Lembeli akidai kuwa kifungu namba nane cha hati ya kesi
aliyofungua ndio msingi wa kesi hiyo
lakini kulingana na pingamizi lililowasilishwa anaiachia sheria ichukue mkondo
wake.
Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mh.Victoria Makani
baada ya kusikiliza pande zote mbili ameahirisha kesi na kuitaja tarehe nane
mwezi huu siku ya ijumaa saa tatu asubui kuwa mahakama itatoa hukumu juu ya pingamizi
hilo ili kuruhusu kesi ya msingi kuanza kusikilizwa.
0 comments:
Post a Comment