Watu watano wa familia moja wamefariki dunia baada
ya kusombwa na maji ya mto katika kijiji cha Nyarubanda katika halmashauri ya
wilaya ya Kigoma wakati wamelala.
Kwa mujibu wa Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini
PETER SERUKAMBA tukio hilo limetokea kufuatia mvua kubwa zilizonyesha kwa saa
nane na kusababisha Mto Nkonko uliopo Vijiji vya Nyarubanda na Mkigo kujaa maji
na kuwasomba watu hao.
Amesema tayari maiti tatu zimepatikana huku jitihada
za kutafuta maiti nyingine zikiwa zinaendelea na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Kigoma Bwana FERDINAND MTUI amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa uchunguzi
na kusaidiana na wananchi kutafuta miili zaidi.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyarubanda NORBERT
MCHEMWA amesema familia hiyo ilikuwa katika shghuli za kawaida za shamba na
baada ya kuona mvua walikaa ndani ya nyumba ya muda waliyojenga shambani hapo
lakini mto ulikatika na mkondo wa maji kuipitia nyumba hiyo pamoja na kuwasomba
watu wote waliokuwemo.
0 comments:
Post a Comment