MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora Chini ya Jaji Sam
Rumanyika leo Januari 14, 2016 imetupilia mbali mapingamizi ya Wakili wa
serikali yaliyowasilishwa na kujadiliwa Jan11, 2015 katika mahakama hiyo.
Katika mapingamizi ya serikali Wakili wa serikali
kwa niaba ya msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria wa serikali aliweka
mapingamizi na kutaka mahakama itupilie mbali kesi ya Kafulila David kwa madai
kwamba;
1. Hati ya mashtaka haina vifungu vya sheria
vinavyoipa mahakama mamlaka ya kusikiliza kesi hii
2. Ombi la Kafulila kutangazwa mshindi halimo ndani
ya uwezo Wa mahakama kwakuwa mamlaka hayo ni ya Tume ya uchaguzi
3. kwamba ombi la Kafulila kwamba mahakama
ipitie fomu za matokeo haitambuliki kisheria.
Katika uamuzi wa MAHAKAMA, Jaji Rumanyika
amesema baada ya kusikiliza na kuchambua mapingamizi na utetezi wa Wakili wa
Kafulila imeamua kuwa;
1. Hoja kwamba hati ya mashtaka haina au
haijaweka sheria I nayoipa mamlaka mahakama kusikiliza na kuamua KESI hii
haina msingi kwakuwa kwanza kesi ya uchaguzi sio sawa na maombi ya kawaida na
zaidi sheria ya uchaguzi ya 2015, kifungu110 kimesisitiza wazi kuwa
mahakama kuu ndio yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za uchaguzi na hivyo haikuwa
na ulazima kutaja ukweli ulio hayana.
2. Hoja kwamba mahakama haina uwezo wa kutangaza
mshindi haina msingi kwasababu sheria ya uchaguzi ya 2015 kifungu112 kimeweka
wazi mamlaka ya mahakama kuwa ni pamoja na kutangaza mshindi alochaguliwa na
hivyo Kafulila Ana haki kuomba ombi hilo.
3. Kuhusu pingamizi kuwa ombi la Kafulila la
kuomba kupitiwa fomu 21B za kila kituo, MAHAKAMA imelekeza kuwa dhana ya
ombi hilo inamezwa na ombi la kutangazwa mshindi hivyo halina sababu kuwepo.
Baada ya maelekezo na maelezo hayo, Mahakama
haioni sababu ya kufuta kesi ya Kafulila David Kama ilivyombwa na wakili wa
serikali na badala yake Kesi itaendelea January 28, 2015.
0 comments:
Post a Comment