Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
wa Tanzania Bw Augustine Mahiga amesema serikali ya Burundi bado inaunga mkono
mazungumzo ya amani yenye lengo la kukomesha mgogoro nchini Burundi.
Bw Mahiga amesema Burundi haipingi mazungumzo
yaliyoanzishwa na nchi jirani, na taarifa zilizopo ni kuwa serikali ya Burundi
bado inajiandaa kwa ajili ya mazungumzo hayo, na kutofika kwa ujumbe wa
serikali kwenye mazungumzo ya Arusha sio ushahidi kuwa Rais Nkurunziza anapinga
juhudi za upatanishi za jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi nyingine.
Bw Mahiga amesema serikali ya Burundi imeomba
kusogeza mbele tarehe ya mazungumzo na kupewa muda wa kutosha kufanya
majadiliano kuhusu wajumbe na ukubwa wa ujumbe unaowakilisha pande mbalimbali
zinazozozana.
0 comments:
Post a Comment