Maumivu chuni ya kitovu hutokea kama ifuatavyo:
Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na
kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale
ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne
na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya
kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa
kwa marefu.
Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake
wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia
yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu
vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala
kifudifudi.
Maumivu chini ya kitovu yanaashiria matatizo gani kwa
wanawake?
(i)
Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na
machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye
amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya
uzazi na wakati huo huo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au
upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana
na kujaa maji machafu.
(ii)
Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii
husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea mwanamke
maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye anamaumivu chini ya
kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi mfano hedhi kukoma au kutokuwa
na mpangilio maalum kunauwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya
mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na
kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili
ya kichomi.
(iii)
Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na
kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia
maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huo huo
akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kunauwezekano akawa na
PID hasa hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla
haijafikisha miezi mitano.
(iv)
Afya mbovu ya kibofu cha mkojo
ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI).
Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana
na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara. Itaendelea wiki
ijayo
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume
huashiria nini?
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume
huashiria pia tatizo la tezi dume liitwalo Prostatitis yaani kuvimba kwa
tezi dume. Maumivu haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo hili
hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na
umri ukiwa unaelekea miaka 50 au zaidi. Dalili nyingine ambatano ni kutoa
haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana tofauti na kawaida, ikiambatana na
maumivu ya kiuno na mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na
usaha na damu, maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni, na damu katika
maji ya uzazi (semen)
Kwa wanaume, maumivu haya ya chini
ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo kitaalamu hujulikana kwa jina la Hernia
ambapo waswahili tunaita ngiri. Mwanaume anaposikia maumivu haya ya chini ya
kitovu ikiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine
kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea, ni dalili ya ugonjwa huu ambao
huharibu ubora wa uzalishwaji wa mbegu za kiume ambazo zaweza kuzalishwa chache
au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vywa mwanamke na
hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume
kama ilivyo kwa wanawake huashiria tatizo la maambukizi katika mfumo wa haja
ndogo yaani (Urinary Track Infection/UTI) ambapo dalili zake ni kama zile za
mwanamke hapo juu.
Hitimisho.
Vipimo na tiba vyahitajika mapema
bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata
wa chakula
ano ilipongia madarakani na kufanya mabadiliko
kwenye uongozi wa TRA na kudhibiti ukusanyaji mapato.
Ni jambo la kupongezwa kwani ni miaka mingi viongozi
walijenga dhana kuwa Tanzania ni maskini isiyoweza kujitegemea.
Matokeo yake wananchi wamekuwa wakiishi kwa mateso
makubwa kwa kuaminishwa kuwa nchi kama Tanzania ni maskini na ilipaswa
kutegemea misaada ya nchi za nje.
Na hiyo ndiyo ikawa staili ya viongozi wengi
kuhalalisha safari za kwenda nchi za kigeni kusaka misaada `eti’ kwa kuwa nchi
yetu ni maskini.
TRA imepata mafanikio haya baada ya serikali kubana
eneo moja tu la bandari katika kuhakikisha watu wanalipa kodi kihalali. Mamlaka
hiyo imevunja rekodi ya kukusanya mapato ya awamu ya nne, ambayo kiwango chake
cha juu kilikuwa kati ya Sh. bilioni 800 na bilioni 900.
Tunaupongeza uongozi wa TRA na serikali katika
kuhakikisha kuwa kiwango kikubwa cha mapato kinakusanywa.
Fedha hizo tayari zimeanza kutumika kupunguza makali
ya maisha kwa Watanzania mathalani, zile zilizokusanywa Novemba
zimeelekezwa kusaidia utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. John Magufuli, ya kutoa
elimu bure.
0 comments:
Post a Comment