Mshambuliaji mmoja ameripotiwa kuuawa wakati
alipokuwa akijaribu kuingia kwenye kituo cha polisi na bomu katika mji mkuu wa
Paris nchini Ufaransa.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Ufaransa
Pierre-Henri Brandet, alitoa maelezo kwenye kituo cha BFMTV na kusema kwamba
mshambuliaji alikuwa amevaa vilipulizi na mkononi alikuwa amebeba kisu.
Mshambuliaji huyo pia alikuwa na nyaya za umeme
pamoja na bomu.
Polisi wametambulisha tukio hilo kuwa kama ''jaribio
la shambulizi la kigaidi'' lililotaka kutekelezwa katika kipindi cha
maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa mashambulizi ya
Charlie Hebdo.
0 comments:
Post a Comment