Tunda hili linapotengenezwa kama kinywaji (juis) husaidia kuondoa
maumivu ya tumbo na kuponya vidonda vya tumbo pamoja na kurekebisha
udhaifu mwingine tumboni.
Tabibu Abdallaah Mandai anaeleza kuwa tunda hilo husaidia kuongeza nguvu za mwili na ubongo sambamba na kujenga neva na fahamu.
Aidha, mtaalam huyo anabainisha kwamba, tunda hilo pia huweza
kumpatia mtu uwezo mzuri wa kuona, huku majani yake yakielezwa kuongeza
damu na kusheheni vitamin A, B, C na E.
Tabibu Mandai anasema
kuwa, vyakula kama nyama husababisha 'uric acid' nyingi mwilini, ambayo
husababisha magonjwa mengi mwilini, hivyo tunda hili huweza kusafisha
hiyo na kuitoa nje na kuondoa magonjwa pia.
“Tunda hili
hufanya vizuri sana kwa magonjwa hayo na kuyamaliza, lakini pia husaidia
wanawake katika kuifanya hedhi iende vizuri kila mwezi,” alisema mtaalam huyo.
Pia
majani yake yanapochemshwa kama chai na mtu kunywa husaidia kuondoa
matatizo mwilini, ikiwa ni pamoja na uchovu, udhaifu na kujisikia ovyo,
kuumwa kichwa, koo (throat), tumbo, mapafu na uvimbe.
Hali kadhalika, unapotafuna majani yake husaidia kutibu vidonda vya mdomo (ufizi) na kuimarisha meno pamoja na kuondoa maumivu.
Pamoja
na hayo, Tabibu Mandai anasema parachichi huweza kutumika hata katika
masuala ya urembo, ambayo ni pamoja na kukuza nywele na kuokoa wale
wenye tatizo la nywele zinazoanguka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment