Baadhi ya wanawake wanapokaribia kuingia katika siku zao misuli hubana na maumivu ya mapaja na miguu.
Lakini wakati mwingine hali huwa inakuwa mbaya zaidi ambapo
mhusika anapata maumivu makali ya mgongo, tumbo na hata maumivu wakati
wa kutoa damu. Sasawataalam wanasema kwamba tangawizi inaweza kuwa suluhisho la tatizo la maumivu hayo makali wakati wa hedhi kwako mwanamke.
Unachotakiwa kufanya ni kupondaponda tangawizi mbichi, kisha chemsha maji ya kutosha kwa dakika kumi. Ongeza sukari kidogo halafu chuja.
Tumia glasi moja ya maji hayo mara tatu kwa siku hususani mara baada ya kula.
Matibabu haya ni vyema yakaanza siku tatu kabla ya hedhi na kipindi chote cha hedhi.
0 comments:
Post a Comment