Juisi ya embe husaidia sana kuleta uoni mzuri kwa sababu juisi hiyo
ina vitamin A ambayo huimarisha sana afya ya macho na kuwasaidia wale
wenye macho makavu na wenye uoni hafifu wakati wa usiku 'blindness'.
Matumizi
ya juisi ya embe pia huwa na faida kubwa kwa afya ya ngozi, unachopaswa
kufanya ni kupaka makapi ya embe usoni na kukaa nayo kwa muda
usiopungua dakika kumi, baada ya dakika hzio kupita utaosha uso kwa
maji yanayotirirka husani yanayotoka bombani. zoezi hilo litakusaidia
sana kuonekana na ngozi nzuri pamoja na kutibu shida ya chunusi pia.
Juisi
ya embe inapotumika bila kuwekwa sukari huwa ni nzuri sana kwa watu
wenye shoda ya kisukari kwani huenda kusaidia kurekebisha sukari ya
mwili kuwa vizuri na kurekebisha mapigo ya moyo kuwa sawa na kuondoa
sumu hatari mwilini
Juisi hii pia inasifika kwa kuimarisha mfumo
wa umeng'enyaji wa chakula mwilini, pamoja na kusaidia sana kuondoa
shida ya ukosefu wa choo hasa pale unapopata juisi yenye mchanganyiko wa
embe na nanasi huwa nzuri zaidi kwa shida hiyo.
Ndani ya juisi
ya embe huwa kuna vitamin C, na vitamin A pamoja na 'carotenoids' ambazo
zote zinapokuwa kwa pamoja husaidia sana kuimarisha kinga za mwili.
Pia ndani ya juisi ya embe hupatikana vitamin B, E. K pamoja na madini calcium, potassium, magnesium, phosphorus na iron.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment