Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Jamal
Malinzi amempongeza mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya TP
Mazembe ya Congo DR kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji
wanaocheza ndani.
Samatta ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa
wachezaji wanaocheza Afrika baada ya kwashinda Robert Kidiaba (Congo DR)
alieshika nafasi ya pili na Bounedjah Baghdad (Algeria) aliyeshika nafasi ya
tatu.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Samatta amekua mchezaji wa
kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kushinda tuzo kubwa barani Afrika.
Pamoja na kushinda tuzo hiyo, Samatta pia
amejumuishwa katika kikosi bora cha wachezaji wa Afrika kwa mwaka 2015 sambamba
na Robert Kidiaba (Congo DR), Sergie Aurier (Ivory Coast), Aymen Abdenmor
(Tunisia), Mohamed Meftah (Algeria), Sadio Mane (Senegal), Yaya Toure (Ivory
Coast), Yacine Ibrahim (Algeria), Andrew Ayew (Ghana), Mbwana Samatta
(Tanzania), Pierre-Emercik Aubameyang (Gabon) na Baghdad Bounedjah (Algeria).
Mshambuliaji Mbwana Samatta alieyambatana na Katibu
Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine wanatarajia kuwasili nchini leo saa 8 usiku kwa
shirika la ndege la Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment