Abu Muhammed al-Adnan, ambaye ni msemaji wa kundi la
kigaidi la DAESH nchini Iraq, anadaiwa kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya angani
yaliyotekelezwa wakati wa operesheni.
Wizara ya ulinzi ilitoa maelezo na kuarifu
kujeruhiwa kwa Adnan siku chache zilizopita, katika mashambulizi ya angani
yaliyotekelezwa na ndege za kivita za jeshi la Iraq kwenye eneo la Barwane
lililoko mjini Anbar.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Adnan alifikishwa
kwenye hospitali moja ya eneo la Hayt kwa ajili ya matibabu baada ya kupoteza
damu kutokana na majeraha.
Baadaye Adnan aliweza kusafirishwa Mosul chini ya
ulinzi mkali.
Nchi ya Iraq imekuwa ikikumbwa na mizozo ya kundi la
kigaidi la DAESH linalotaka kutawala baadhi ya maeneo ya Iraq na Syria tangu
mwezi Juni mwaka 2014.
Vikosi vya majeshi ya kimataifa vinavyoongozwa na
Marekani vimekuwa vikitekeleza operesheni ya angani dhidi ya DAESH kwa kipindi
cha zaidi ya mwaka mmoja.
0 comments:
Post a Comment