Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), limetuma salamu
za rambirambi kwa kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Suleiman “Morocco” kufutia
kifo cha baba yake mzazi Suleiman Ally Hemed kilichotokea juzi kisiwani
Zanzibar.
Katika salamu hizo za rambirambi, TFF imewapa pole
wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja na familia ya marheemu
katika kipindi hiki kigumu cha maombeloezo.
Aidha pia TFF imetuma rambirambi (ubani) wa shilingi
laki mbili (200,000) kwa familia ya kocha Hemed Moroco kufuatia kifo cha baba
yake Suleiman Ally.
Mazishi ya marehmu Suleiman Ally Hemed mefanyika
jana jioni mjini Zanzibar
0 comments:
Post a Comment