Mabingwa wa Tanzania Bara Timu ya Yanga,
wamefanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi
ya Mtibwa mabao ambayo yamefungwa na wachezaji Aboubakar na Malimi Busungu na
kuwa kinara wa kundi B la michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kujikusanyia
jumla ya pointi 7.
Katika mchezo mwingine wa mapema wa kufuzu hatua ya
nusu fainali, timu ya mafunzo imeichapa Azam FC 2-1 kwa ushindi usio na faida
kwa timu hiyo baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo kwa uchache wa pointi.
Yanga sasa watacheza nusu fainali na mshindi wa pili
wa Kundi A huku Mtibwa Sugar nao wakikutana na mshindi wa kundi hilo.
Kundi A linamaliza mechi zake leo Ijumaa kwa Timu ya
Jamhuri kuchuana na URA na Simba ikicheza na JKU huku kila timu ikiwa ina
nafasi ya kutinga nusu fainali ikipata matokeo mazuri ingawa sare kwa Simba
itawafikisha nusu fainali.
URA na Jamhuri zinahitaji ushindi.
0 comments:
Post a Comment