Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamini William Mkapa Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam alipomtembelea January 7,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam January 7,2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo January 7,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Warioba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Mkapa
amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa
na watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.
Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa
yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo
atahitajika kufanya hivyo.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Warioba pamoja na kumtakia heri ya Mwaka Mpya, amempongeza Rais Magufuli kwa
jinsi alivyoanza kazi vizuri hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato,
kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu
wananchi yakiwemo afya na maji.
Jaji Warioba ameongeza kuwa Watanzania wote wanapaswa
kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya, ambazo ni kukomesha
rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.
"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije
tukamuachie, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo,kama ni mambo
ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee
yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini watanzania wote tushughulike na matatizo
hayo" alisisitiza Jaji Warioba.
0 comments:
Post a Comment