Image
Image

Waziri Simbachawene amsimamisha kazi kaimu afisa biashara wa manispaa ya ilala kwa upotevu wa mapato ya serikali



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumsimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala Bw.Dennis. N. Mrema kuanzia leo kwa kosa la kusababisha upotevu wa Mapato ya Serikali kutokana na urasimu wa kukusudia, mazingira ya rushwa na uzembe katika utoaji wa leseni za Biashara.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ameelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Ilala na nafasi yake kukaimiwa na mtu mwingine ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zilizotolewa dhidi yake. Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI amefikia uamuzi huu baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa Wafanyabiashara ambao wamemlalamikia Mtendaji huyu kwa ukiukwaji wa Sheria,
Kanuni na Taratibu za utoaji wa Leseni za Biashara,Urasimu na Mazingira ya rushwa.

Aidha katika uchunguzi wa awali uliofanyika kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ulibaini mambo mbalimbali ikiwemo,Ukiukwaji
wa Makusudi wa Sheria, Kanuni  na Taratibu  za utoaji wa Leseni za Biashara,Kutoa Leseni za Biashara zaidi ya 843 bila
kuwa na Vyeti vya uthibitisho wa Walipa kodi ‘Tax ClearanceCertificates” hivyo kuikosesha Serikali Kodi ya Mapato,Kukaa na fomu za Wafanyabiashara 336 kwa muda mrefu bila sababu za msingi,Kukiuka mwongozo wa Mkataba wa Huduma kwa wateja ambao unamtaka Afisa Biashara kutoa Leseni za Biashara ndani ya siku 2 hadi 3 baada ya muombaji kuwasilisha maombi yake ya kupatiwa Leseni ya Biashara.

Aidha, Mheshimiwa Waziri wa Nchi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI amewaagiza Maafisa Biashara wote nchini watoe huduma za Leseni kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu , kuacha urasimu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment