Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi,Mhe.William
Lukuvi ameliagiza shirika la nyumba la taifa, NHC,kukusanya fedha za madeni ya
shirika hilo kutoka kwenye taasisi za serikali ambazo zimelimbikizwa kwa muda
mrefu bila kulipwa licha ya taasisi hizo za umma kuendelea kutumia huduma za
shirika hilo.
Waziri lukuvi ametembelea ofisi za shirika la nyumba la
taifa, mkoani mbeya na kuzungumza na wafanyakazi wa shirikika hilo ambapo
meneja wa NHC mkoa wa mbeya, Juma Kiaramba akamweleza matarajio ya shirika hilo
ya kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Akizungumzia changamoto za shirika hilo, kiaramba amemweleza
waziri Lukuvi kuwa, shirika linakabiliwa na tatizo la wateja wake kutolipa
fedha za pango la nyumba zake kwa wakati,na kuwataja baadhi ya wadaiwa sugu
ambao ni taasisi za serikali.
Akizungumza na wafanyakazi hao,waziri Lukuvi amewapongeza
kwa kazi nzuri wanayoifanya,lakini akawaagiza kuongeza jitihada katika
kukusanya madeni ya shirika hilo hasa yale ambayo shirika linazidai taasisi za
serikali.
0 comments:
Post a Comment