Beki wa Ivory Coast, Kolo Toure (kulia) akipambana na Mbwana
Samatta wa Taifa Stars wakati wa mechi ya kuwania nafasi ya kushiriki
kombe la dunia 2014.
Mwanasoka
raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC) Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa
Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika, wakati tuzo ya mwanasoka bora
barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata
kabumbumbu katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Tuzo
hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika
almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia leo mjini Abuja nchini
Nigeria. Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu
ya Cameroon. Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory
Coast.
Mbwana Ally Samatta akiwa amejifunika bendera ya Taifa kwa furaha baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa afrika anayechezea barani Afrika.
Kocha
bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda
kwa mwaka wa pili mfululizo wakati Klabu bora ya soka barani Afrika ni –
TP Mezembe, kutoka DR Congo ambapo mwanasoka bora wa kike Afrika ni
Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon na Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary
Gassama kutoka nchini Gambia
Tuzo
hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii
maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli
kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria
Omowumi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment