SERIKALI imesema kama Shirika la Afya Duniani (WHO),
litapitisha matumizi ya dawa mpya ya ugonjwa Ukimwi wataitumia,lakini kwa sasa
haiwezi kuzungumzia tafiti za ugonjwa huo ambazo zipo nyingi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John, alisema kwa sasa zipo tafiti
nyingi, lakini wao kama wizara wanasubiri mwongozo kutoka WHO ambao ndiyo
unathibitisha ubora wa dawa na matumizi yake.
“Zipo tafiti nyingi tunazisikia zinafanyika, lakini
hili la Ukimwi ni mapema mno kulizungumzia ila kinachohitajika ni kusubiri
mwongozo wa WHO ambao ndio wanatuongoza kwenye orodha ya dawa na matumizi yake
katika magonjwa mbalimbali,” alisema John.
Juzi mashirika mbalimbali ya habari yalitoa taarifa
juu ya utafiti mpya wa dawa ya mseto ya kimiminika ijulikanayo kama PrEP ambayo
inatarajiwa kuleta faraja kwa wenza ambao mmoja anaishi na virusi vya Ukimwi
huku mwingine akiwa hana.
Dawa hiyo inadaiwa tayari imeanza kutumika kwa
baadhi ya mashoga nchini Uingereza na Marekani ambapo huweza kuondoa hatari ya
kuambukizwa hadi asilimia sifuri. Pia itaondoa changamoto iliyokuwapo katika
njia namba moja ikiwa pamoja na kujikinga na virusi vya Ukimwi, yaani kutumia
kondomu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Kutokana na matumizi ya kondomu wenzi hao walikuwa
hawawezi kupata watoto bila uwezekano wa kuhatarisha afya ya mwenzi ambaye hana
VVU.
0 comments:
Post a Comment