Utafiti mpya wa tiba unasema watoto milioni mbili
nukta sita wanafariki kabla ya kuzaliwa duniani kote kila mwaka, na theluthi
mbili ya vifo hivyo vinatokea barani Afrika.
Akichapisha ripoti yake katika jarida la The Lancet,
jopo la wataalamu kutoka chuo cha afya mjini London limesema kumekuwa na
maendeleo finyu katika kupunguza idadi ya vifo vya watoto kabla ya kuzaliwa
licha ya kuwa vinaweza kuepukika.
Miongoni mwa taarifa za kushangaza katika ripoti
hiyo, ni kwamba itachukua zaidi ya miaka mia moja na sitini kwa mwanamke wa
kawaida anaetoka katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara kuweza kujifungua
mtoto aliyehai kama ilivyo kwa mwanamke katika nchi zenye pato la juu.
Katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara, utafiti
huo unasema, asilimia sitini ya vifo vya watoto wanaozaliwa vinatokea katika
maeneo ya vijijini.
Katika bara la Afrika, nchi ya Nigeria ndio
inaongoza kwa idadi kubwa ya vifo hivyo, huku ikiwa na zaidi ya vifo mia tatu
katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ya ujauzito.
Miongoni mwa habari njema ni nchi ya Rwanda ambayo
imeweza kubadilisha mwelekeo na kupunguza idadi ya vifo hivyo.
Waandishi wa ripoti hiyo wanasema, uboreshaji
umefanyika zaidi katika afya ya kina mama na vifo vya watoto, lakini sio katika
kupunguza vifo vya watoto ambao hawajazaliwa.
Wamesema, watoto hawapaswi kuzaliwa katika ukimya na
wazazi wao hawapaswi kuomboleza kimya kimya.
0 comments:
Post a Comment