Polisi
nchini Uganda wamemkamata tena aliyekuwa mgombea urais na kiongozi wa chama cha
upinzani cha FDC cha Uganda Bw. Kizza Besigye ili kuepusha machafuko baada ya
uchaguzi mkuu.
Bw.
Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi wa rais, na kutoa wito wa kufanya
maandamano ya amani. Amesema uchaguzi huo haukuwa wa haki na wazi, na unapaswa
kuangaliwa na tume maalum ya kimataifa.
Habari
zinasema, baadhi ya nchi za magharibi zinadai kuwa uchaguzi huo uliofanyika
alhamis iliyopita ulitawaliwa na rushwa na matumizi mabaya ya polisi. Lakini
rais mteule wa Uganda Yoweri Museveni amekanusha madai hayo.
0 comments:
Post a Comment