Wachezaji wa safu ya kiungo cha kati wa Arsenal
Mesut Ozil na Aaron Ramsey pamoja na kipa Petr Cech watarudi katika mechi ya vilabu
bingwa Ulaya dhidi ya mabingwa watetezi Barcelona siku ya jumanne.
Wachezaji hao walipumzishwa katika mechi ya kombe la
FA siku ya Jumamosi dhidi ya Hull City.
Barca itamrudisha katika kikosi chake beki Gerard
Pique,ambaye alipumzishwa katika ushindi dhidi ya Las Palmas na kiungo wa kati
Sergio Busquets ambaye alikuwa akihudumia marufuku.
''Tunahitaji kuwa na mwelekeo katika mechi hiyo kwa
pamoja ili kuwa na fursa ,''alisema mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger.
Arsenal iliondolewa na kilabu ya Monaco katika
mchujo wa msimu uliopita.
Walipoteza kwa mabao 3-1 katika uwanja wa
Emirates,lakini wakashindwa kufuzu baada ya kushinda maba 2-0 ugenini kutokana
na bao la ugenini.
''Ni fursa kuonyesha kwamba tumepata funzo,kwa
sababu tulijipatia kibarua kigumu baada ya mechi ya nyumbani,''alisema.
0 comments:
Post a Comment