Mchezaji wa klabu ya Trabzonspor, Salih Dursun,
alitolewa nje kwa kumuonyesha mwamuzi kadi nyekundu wakati wa mchezo
waliofungwa mabao 2-1 na Galatasaray katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 86 ya mchezo, klabu
hizo zikiwa zimetoshana nguvu 1-1, baada ya mwamuzi Denis Bitnel kumuonyesha
kadi nyekundu ya moja kwa moja Luis Cavanda kwa kufanya madhambi ndani ya eneo
la hatari. Aidha, aliwazawadi Galatasaray penalti.
Trabzonspor walikuwa tayari wamesalia wachezaji tisa
uwanjani kabla ya kutokea kwa kisa hicho.
Wachezaji wa Trabzospor walimzingira mwamuzi kupinga
kadi hiyo.
Ni wakati huo ambapo Dursun alimnyang’anya refa kadi
nyekundu aliyokuwa nayo na kumuonyesha kadi hiyo hatua ambayo ilipelekea na
yeye kufukuzwa uwanjani.
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuingia katika
mizozo na waamuzi, kwani Novemba mwaka jana mwenyekiti wao Ibrahim
Haciosmanoglu alifungiwa siku 280 baada ya kuwafungia waamuzi wanne uwanjani
kwa kushindwa kutoa penati kwa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment