Ligi ya
Uingereza ni mpizani mkubwa wa Barcelona ikilinganishwa na Real Madrid,amesema
rais wa kilabu hiyo Josep Maria Bartomeu.
Kilabu
20 za ligi kuu ya Uingereza zitaanza kugawanya kitita cha pauni bilioni 5.136
za matangazo ya moja kwa moja kuanzia msimu ujao.
''Timu
za ligi ya Uingereza zitakuwa na ubabe wa kifedha kuanzia sasa na tuna
wasiwasi,''Bartomeu aliiambia BBC Sports.
Kilabu
ya Barcelona inakabiliana na Arsenal katika ligi ya vilabu bingwa Ulaya siku ya
Jumanne.
Kikosi
cha Luis Enrique kitaanza awamu ya kwanza ya kombe hilo katika uwanja wa
Emirates kikiwa hakijafungwa katika mechi 32 za ligi na zile za kombe la ligi
hiyo huku kikitaka kushinda kombe hilo kwa msururu.
Kilabu
kubwa za Uhispania -Barca na Real Madrid,zilijadili kuhusu mikataba yake ya mechi
za ligi hiyo zinazoonyeshwa moja kwa moja katika runinga lakini sasa zimezuia
kufanya hivyo kupitia sheria mpya ya Uhispania.
0 comments:
Post a Comment