Klabu ya Manchester united jana ilifanikiwa kutinga hatua ya
robo fainali ya michuano ya FA baada ya kuvuna ushindi mnono dhidi ya
Shrew-Sbury Town wa mabao 3-0.
Mabao ya Manchester united yamefungwa kupitia wachezaji wake
Chris Smalling , Juan Mata na Jesse Lingard .
Baada ya ushindi huo sasa Manchester united itakutana na
West Ham United katika hatua ya robo fainali Mechi ambazo zinatarajia kuchezwa
wikiendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.
Chelsea itamenyana na Everton katika mchezo wa Robo Fainali
baada ya kuiondoa Manchester City, Crystal Palace wakiongozwa na wao watasafiri
kuikabili Reading , Watford watakuwa wageni kati ya Arsenal au Hull
0 comments:
Post a Comment