Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa
taarifa likilaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea mjini Damascus na Homs,
Syria na kusema uwepo wa kundi la IS umeathiri vibaya utulivu na hali ya haki
za binadamu nchini Syria. Baraza hilo pia limetoa wito kwa pande zote kuanza
tena mazungumzo ya amani haraka iwezekanavyo.
Habari kutoka Ikulu ya Ufaransa zinasema viongozi wa
Ufaransa, Marekani, Ujerumani na Uingereza jana walijadiliana kwa njia ya simu
kuhusu makubaliano ya kusimamisha vita nchini Syria yaliyofikiwa kati ya
Marekani na Russia na kutarajia kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa haraka.
Wakati huohuo, waziri wa maridhiano ya kitaifa wa
Syria Bw Ali Haidar amesema, serikali ya Syria imekubali makubaliano
yaliyofikiwa kati ya Marekani na Russia, lakini makubaliano hayo hayataathiri
mapambano ya Syria dhidi ya ugaidi
0 comments:
Post a Comment