Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa
Mataifa amesema madola makubwa yanakiuka haki za nchi zinazoendelea kutokana na
mtazamo wao wa kujifanyia mambo yatakavyo na wa upande mmoja.
Gholamali Khoshroo ambaye alikuwa akihutubia Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kwa niaba ya nchi wanachama wa Harakati ya Nchi
Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) amesema maadhimisho ya miaka 70
ya kuundwa kwa umoja huo ni fursa ya kuilinda Hati ya Umoja wa Mataifa ikiwa
ndiyo njia pekee ya kudhamini amani na usalama duniani. Ameongeza kuwa kutojali
nchi zilizoendelea haki za kiuchumi na kijamii za nchi zinazoendelea kumeitia
hatarini amani na usalama wa dunia.
Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa
Mataifa ameongeza kuwa kwa mtazamo wa NAM, kuheshimu haki ya mamlaka ya utawala
ya taifa, usawa kwa nchi zote, kujitawala na kupinga utumiaji mabavu na au
vitisho katika uhusiano wa kimataifa ni usuli na mambo ya msingi ambayo yana
ulazima wa kuheshimiwa na nchi zote.
Khoshroo amebainisha kuwa haipasi kuchukua hatua za upande
mmoja za uadui wa kiuchumi dhidi ya mataifa kwa lengo la kubana uhuru na
kujitawala kwa baadhi ya nchi wanachama wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na
Siasa za Upande Wowote.
Aidha amesisitiza kwa mara nyengine juu ya msimamo wa NAM
kwamba Hati ya Umoja wa Mataifa ina uwezo na njia kadhaa za kutatulia migogoro
ya kimataifa; hivyo kuna ulazima wa kuzitumia zaidi fursa za sura ya sita na ya
nane ya hati hiyo na kwamba utumiaji wa sura ya saba ikiwa ni njia ya mwisho ya
utatuzi ufanyike pale tu amani na usalama wa kimataifa zunapokuwa zimekabiliwa
na tishio kubwa na la kweli.../
0 comments:
Post a Comment