HAKUNA mjamzito atakayejifungua kwa shida katika Hospitali
ya Muhimbili” ni ahadi aliyoitoa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto leo wakati akiratibu zoezi la uwekaji wa vitanda katika
Wodi ya Wazazi.
Akizungumza katika kipindi moja kwa moja ‘live’ cha ‘Super
Mix’ cha East Africa Radio amesema, kufanyika kwa zoezi hilo ni kufuatia agizo
la Rais John Magufuli la kubadili matumizi ya Wizara ya Afya, Kitengo cha Afya
ya Uzazi na Mtoto kuwa kuwa wodi ya wazazi.
Ummy amesema, Rais Magufuli anataka suluhisho la matatizo na
sio michakato ya utatuzi na kwamba, atahakikisha wizara yake inakwenda sambamba
na yale ambayo rais angependa kuyaona katika utawala wake wa awamu ya tano.
“Mimi ni mwanamke, na nimeshajifungua mara mbili, najua
uchungu wa uzazi, sitakubali wakinamama wateseke kwa kujifungua, leo mama
atalala kitandani,” amesema.
0 comments:
Post a Comment