Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh. Prof. Makame
Mbarawa amewaonya vikali baadhi ya watumishi wa kampuni ya simu Tanzania ( TTCL
), wanaojifanya kuwa mawakala wa kampuni nyingine za simu kuacha mara moja
tabia hiyo, la sivyo atawafukuza kazi kwani ni heri kampuni ikabaki na
watumishi wachache waadilifu kuliko kuwa na wafanyakazi wengi wasio waaminifu
wanaoendelea kuihujumu TTCL.
Prof. Mbarawa ametoa onyo hilo baada ya kutembelea na
kujionea hatua za ujenzi wa mradi wa upanuzi wa mkongo wa taifa awamu ya tatu
katika vituo vya Ghana na Mwanza telephone house eneo la posta jijini
Mwanza.
Meneja wa TTCL mkoa wa Mwanza Johnbosco Kalisa kilio chake
ni madeni ya wateja sugu zikiwemo idara za serikali.
Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL na posta mkoani Mwanza
wanaeleza kilio chao kwa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh. Prof.
Makame Mbarawa juu ya changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wao wa kazi
za siku kwa siku.
Pamoja na TTCL kupewa jukumu la kuongoza mkongo wa taifa kwa
kutumia teknolojia ya Optical Fibre, ambapo Mwanza ni kiungo kikuu cha kanda ya
ziwa na nchi jirani, ulinzi na usalama wa mkongo huo bado unakabiliwa na hujuma
zinazodaiwa kufanywa kwa makusudi na baadhi ya watu pamoja na wakandarasi wa
barabara wanapokuwa kazini.
0 comments:
Post a Comment