Mshauri wa masuala ya kisiasa wa Rais Bashar al Assad wa
Syria amesema kuwa,madai ya Marekani kwamba inapambana na ugaidi ni uongo ulio
wazi.
Bi Bouthaina Shaaban ambaye pia ni mshauri wa Rais wa Syria
katika masuala ya habari amesema hayo alipohojiwa na shirika la habari la
Tasnim na kuongeza kuwa, muungano unaodaiwa kupambana na ugaidi unaoongozwa na
Marekani, kamwe hauwashambulii magaidi na wala haujawahi kuzuia magendo ya
silaha zinazopelekwa kwa magenge hayo ya kigaidi.
Bouthaina Shaaban ameongeza kuwa, watu pekee wanaopambana
kikweli kweli na ugaidi huko nchini Syria ni jeshi la Syria, wanamapambano wa
Hizbullah wa Lebanon na Russia.
Mshauri huyo mwandamizi wa Rais wa Syria amesema kuhusu
mazungumzo ya hivi karibuni ya mjini Geneva Uswisi kwamba serikali ya Syria ina
hamu ya kuona mgogoro wa nchi hiyo unamalizika haraka, lakini magenge ya
kigaidi na waungaji mkono wao hususan Saudi Arabia, wanakwamisha mazungumzo
hayo.
Amesema, hadi hivi sasa wapinzani wa serikali ya Syria
wameshindwa kusema ni nani hasa mwakilishi wao halisi; nayo makundi yanayoungwa
mkono na Saudi Arabia kama vile magenge ya kigaidi ya Jaishul Islam na Ahrarush
Sham hayako huru, bali yanasubiri amri tu kutoka kwa Saudia.
0 comments:
Post a Comment