Dar es Salaam.
Ujumbe wenye dalili za ukweli uliojificha ndani ya
mzaha umezaa wimbo mkubwa kati ya wakali wawili wa RnB Tanzania, Benard “Ben
Pol” Paul na Juma “Jux” Khaleed.
‘NAKUCHANA’ ni wimbo mpya wa RnB ambao ndani yake Ben
Pol na Jux wanasikika wakipeana ‘makavu’ kuhusu mambo kadhaa hasi kuhusu
wao, huku kila mmoja akitafuta kile anachoamini ni kona dhaifu ya
mwenzake.
“Nakuchana ilizaliwa baada ya mimi na Jux kwenda studio, na
tulienda studio tulitaka kwenda kurekodi kabisa wimbo rasmi, lakini tukawa
tunajivuta vuta, tukaona bana eh hebu lets just have fun umeona,
sababu tulikaa muda mrefu kama masaa matatu hatujapata kitu. Kwahiyo
tukasema ngoja tujifurahishe (kwa kuchanana) kama watu ambao wanakuwa wana
have fun wanavyochill sehemu, unajua wanazinguana wanafanyaje. Kwahiyo
kwenye ku-have fun ndio tukaandika mstari mmoja mmoja tunau record, tunaandika
mmoja tunau record yaani tumeandika yote kwa pamoja. Kwahiyo hivyo ndivyo
ambavyo ‘Nakuchana’ ilivyozaliwa.” Alieleza Ben Pol kuhusu wimbo huo.
Ben Pol ameongeza kuwa wamelazimika kuitoa ‘NAKUCHANA’ kipindi
hiki kutokana na demo ya wimbo huo kuvuja siku chache baada ya kurekodiwa
na kuonekana kupendwa na mashabiki wengi.
‘NAKUCHANA’ ni wimbo uliopikwa na producer Bob Manecky
wa studio ya A.M Records, na ndio collabo ya kwanza kwa Jux na Ben Pol kufanya.
0 comments:
Post a Comment